HOTUBA YA SHIGONGO YAWAKUNA WAHITIMU MLIMANI SCHOOL OF PROFESSION

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers  Eric Shigongo ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika mahafali hayo akiongoza maandamo maalumu yaliyoandaliwa na chuo hicho, kushoto ni Mkuu wa Chuo, Hassan Ngoma.Shigongo akihojiwa na mwandishi wa chuo hicho cha Professional FM, Shikunzi Haonga ambaye ni mkuu wa kitengo idara ya habari mawasiliano kwa umma (hayupo pichani) ndani ya studio iliyopo chuoni hapo.Shigongo akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa studio hiyo ya chuoni hapo. Wakijadiliana jambo kama wanavyoonekana na mkuu wa chuo hicho.Akitoa vyeti  kwa wahitimu mbalimbali. Shigongo akitunukiwa diploma ya uandishi wa habari mawasiliano ya umma.Shigongo akipigiwa Wimbo wa Taifa baada ya kutunukiwa cheti cha Uandishi wa Habari kutokana na mchango wake mkubwa kwenye tasnia ya habari. Picha ya pamoja na wahitimu wote. Ndugu, jamaa na marafiki wa wahitimu waliofika chuoni hapo kuwapongeza.
Na Haruni Sanchawa
Wahitimu wa Chuo cha Mlimani School Of Profession walipata msisimko mkubwa  baada ya Mkurugenzi  Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo kutoa hotuba ambayo kila mmoja alijiona kuwa anaweza kujikwamua kimaisha kama wakijibidisha katika maisha yao ya kila siku.
Msisimko huo ulikua pale Shigongo alipotoa simulizi ya riwaya ya ombaomba mmoja aliyekuwa akiomba kila siku kwa  kutumia kopo,  kumbe kopo lile ni dhahabu yenye thamani ya mabilioni ya fedha kwenya mahafali ya pili katika chuo hicho.
Mmoja wa wahitumu ngazi ya diploma katika fani ya Habari na Mawasiliani ya Umma, Neema Kisimbo alimpongeza Shigongo kuwa ni kati ya Watanzania wachache waliopewa thawabu  na Mungu hata kama akifa leo atakuwa na la kusema kuhusu alivyoweza kuisaidi jamii.
“Baba huyu ana kipaji lakini mbali na kipaji chake pia kujituma kwake  kumefanya awe na mafanikio makubwa maana maisha ni malengo, si  kweli  kwamba ameenda kwa waganga,” alisema mhitimu huyo.
Katika mahafali hayo, Shigongo aliwatunuku vyetu wahitimu 119 katika Chuo cha Mlimani School of Profession Studies katika mahali yaliyofanyika katika chuo hicho hapo jana Mbezi Kwa Msugur jijini Dar es Salaam.
Wahitumu hao walifunzu katika kozi tofauti ndani ya chuo hicho ambapo kuna baadhi ya walipata ngazi ya cheti na wengine  katika ngazi ya diploma ambapo wote  hao walitunukiwa vyeti hivyo  na mkurugenzi  wa Global Publishars ambaye alikuwa  mgeni rasimi katika mahafali hayo.
Mkurugenzi huyo alitoa vyeti kwa  wahitimu 19 katika ngazi ya cheti kwa fani ya Manunuzi na Ugavi, Fani ya Habari na Mawasiliano ya Uma wahitimu ngazi ya cheti walikuwa 20,  Rasilimali Watu wahitimu 18, ngazi ya cheti wahitimu Uhasibu walikuwa 17 , Uongozi na Biashara ngazi ya cheti sita, Mauzo na Masoko ngazi ya cheti 3, Rasilimali Watu ngazi ya diploma sita , Uongozi wa Biashara diploma 10,  Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya diploma10.
Wengine ni wa Mauzo na Masoko ngazi ya diploma mmoja, Uhasibu ngazi ya diploma sita, Manunuzi na Ugavi ngazi ya diploma  wanne.
Mkuu wa chuo hicho, Hassan Ngoma alimtunuku Shigongo cheti cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ngazi ya Diploma kwa  mchango wake mkubwa katika tasnia ya habari

0 comments: