MZEE MANENTO WA BONGO MUVI ALIKIONA KIFO
KIFO hakina huruma! Wakati
mwili wa aliyekuwa staa mkongwe wa sinema za Kibongo, David Manento
‘Mzee Manento’ (73) ukiagwa nyumbani kwake, Kigogo, Dar, wikiendi
iliyopita na kusafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kwa mazishi,
mwanaye, Godfrey David Manento amesema ni kama mzee huyo alikiona kifo
chake.
Picha tofauti zikionesha aliyekuwa staa mkongwe wa sinema za Kibongo, David Manento ‘Mzee Manento’ (73) enzi za uhai wake.
Godfrey alimwambia mwanahabari wetu:
“Siku za mwisho za mzee wetu kama alikiona kifo kwa sababu alikuwa
akisema jamani mimi naona kama sitapona.”


0 comments: