PICHA ZAIDI ZA AJALI YA HAPPY NATION



Watu 37 wamejeruhiwa mara baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam kupasuka tairi na kupinduka katika eneo la Meta wakati dereva akifanya jitihada za kuikwepa baiskeli katikati ya barabara, Chimala, Mbarali mbeya. Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Happy Nation lenye namba za usajili T. 281 ARR Scania lililokuwa likendeshwa na dereva aliyefamika kwa jina moja la Shabani.Taarifa iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi inasema kuwa basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea mkoani Dar es Salaam. Amesema ajali hiyo imetokea leo Nov 7 majira ya asubuhi baada ya kupasuka tairi la mbele kushoto hali ambayo ilisababisha kuacha njia na kupinduka. 

Amesema mara baada ya kupasuka tairi dereva alishindwa kuimudu nahasa kutokana na eneo lenyewe kuwa na kona kali hivyo aliamua kuligongesha kwenye ukingo wa barabara nakusabisha hali hiyo.Aidha Msangi amesema kuwa kati ya majeruhi hao 29 ni wanaume na wengine 8 nakwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo. 
Amesema kuwa majuruhi Sita kati ya wote hali zao ni mbaya na tayari wamefikishwa katika hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi wakati majeruhi wengine 10 wakiwa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya Chimala.


0 comments: