ANGALIA PICHA MHESHIMIWA LOWASSA AKIZINDUA HELKOPTA YA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA LA MCHUNGAJI GWAJIMA .


Rubani wa helikopta hiyo akijiandaa kuirusha helikopta hiyo.
Helikopta ikiwa hewani.
Hapa ikijiandaa kutua.

Helikopta ya Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima imezinduliwa leo hii katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar na kuhudhuriwa na maaskofu wa makanisa mbalimbali wa madhehebu ya Kikristo nchini.
Uzinduzi huo pia uliohudhuriwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye alikuwa ndiye mgeni rasmi wa uzinduzi huo ulioendana na kukata utepe kisha kuirusha helikopta hiyo hewani kama ishara ya kuanza rasmi kazi yake ambayo ni kutoa msaada wa usafiri wa haraka wakati wa dharura na kuhubiri injili kupitia helikopta hiyo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye viwanja vya kawe lilipo Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa kwenye kwenye jukwaa kuu na mwenyeji wake,Ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Josephat Gwajima (kushoto),Kawe jijini Dar es Salaam leo.Wengine pichani ni Askofu Eliud Isanje (wa pili kulia) na Mchungaji Elifuraha Laswai (kulia).
Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Josephat Gwajima akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Helkopta iliyonunuliwa na Mchungaji huo kwa ajili ya kutoa huduma za kiroho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Helkopta itakayotumiwa na Mchungaji huyo katika kazi zake za kiroho,hafla hiyo imefanyika leo kwenye viwanja vya Kawe,Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na baadhi ya wachungaji waliohudhulia kwenye hafla hiyo.
wakielekea kwenye uzinduzi rasmi wa Helkopta.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Helkopta ya Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kulia kwa Mh. Lowassa).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mtoto wa Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiiingia ndani ya Helkopta hiyo kuashiria kuizindua rasmi kwa safari mbali mbali za kihuduma ya kiroho,itakayotumiwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.
Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiteta jambo na rubani wa Helkopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.
Helkopta iliyozinduliwa ikipaa kuondoka uwanjani hapo na baadae kurudu mara baada ya kuzinduliwa na Mh. Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakati akimuelezea kuhusu vitabu vyake alivyoviandika kabla ya kuvizindua rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kwenye vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto)
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akionyesha moja ya vitabu viliyoandikwa na Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kushoto) wakati alipovizindua rasmi leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima,Kawe jijini Dar es Salaam leo.

0 comments: