MADAHA, ISABELA WAFANYA UFUSKA! USIOFAA KUIGWA HATA KIDOGO JIONEE MWENYEWE HAPA


Mpenzi Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Moja Kwa Moja 

Isabela Mpanda ‘Bella’ na Baby Madaha wakishikana kimahaba.
HAMNAZO? Mastaa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ na Baby Madaha  wamenaswa wakifanya vitendo vichafu maeneo ya Tabata jijini Dar baada ya kupiga masanga ya kutosha mwilini.
Mastaa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda ‘Bella’ na Baby Madaha wakijiachia.
Kwa mujibu wa chanzo, Baby na Bella walifika maeneo hayo juzikati wakiwa wazima kabisa lakini baada ya kufakamia pombe kwa kasi ndipo walipoanza kufanya madudu huku mchumba wa Bella, Luteni Kalama, akiwakimbia na kuwaacha wenyewe.
Isabela Mpanda ‘Bella’ na Baby Madaha wakiwa tungi.
“Walianza kushikanashikana kama wanasagana, wakapakatana huku wakiwa na chupa za pombe wakicheza kwa hisia za kimahaba kama mtu na mtuwe, yani Kalama anatakiwa ajiongeze vinginevyo mkewe mtarajiwa ataharibikiwa,” kilisema chanzo.
Baada ya paparazi wetu kunasa picha tukio hilo kutoka kwa sosi, aliwavutia waya wawili hao kwa nyakati tofauti ambapo walisema hawaoni tatizo katika mambo hayo waliyoyafanya.“Tulikunywa pombe zetu na hatukuwa na tatizo na mtu yeyote kuna shida gani? Hakuna vitendo vibaya tulivyofanya kwa sababu hatukugombana na tulikuwa tuko na  amani na raha zetu,” alisema Baby huku Bella naye akitoa maneno yanayofanana kabisa na hayo ya Baby.

0 comments: