HALI TETE :BAADA YA SHULE YA SEKONDARI YA IFUNDA KUFUNGWA KWA VURUGU UONGOZI WA SHULE HIYO WAWAITA WANAFUNZI 28
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ufundi Ifunda.
Uongozi wa shule ya sekondari ya Ufundi
Ifunda mkoani Iringa imewaita wanafunzi 28 kufika shuleni hapo octoba
2 ikiwa ni baada ya shule hiyo kufungwa kwa muda usiojulikana
kutokana na wanafunzi hao kufanya vurugu kubwa hivi karibuni.
Hatua ya uongozi wa shule hiyo kuwaita
wanafunzi hao imekuja zikiwa ni zaidi ya siku 4 kupita toka shule hiyo
kufungwa kufuatia vurugu kubwa shuleni hapo na kusababisha hasara
kubwa ya mali za shule hiyo.
Makamu mkuu wa shule hiyo Ernest Sakafu ameyasema hayo Leo wakati akizungumza na mtandao wa matukio daima ofisini kwake.
Amewataja wanafunzi wanaotakuwa kufika
shuleni hapo kuwa ni steven Nyiriri, petro Kalolo, Iddi Shaban, John
Zephania, Edwin Rwegoshora, Adinan Mrisho Mtiti, Izengo Dotto, Gaspar
Manyagi, Shemson Amoni ,Halid Omari, Said Sambo, Paschal lusukanija ,
Fred Kidava na Eliji Nguvila
Wengine ni Stambuli Daluweshi, Jackson
Mlowe,Sidi Kayombo,Yusuph Makale , Joseph Antony ,Allan Laurent, Rose
Kayombo, Enoce John, Rashid Kandoro, Abdul Zumo, Petro Silwimba, Joyce
Nestory , Michael Kimario na Athuman Ahamad.
Alisema kuwa kwa sasa shule hiyo imefungwa kutokana na vurugu hizo hivyo shule hiyo itafunguliwa wakati wowote kuanzia sasa.
0 comments: