MHM JOKATE HIKI KIVAZI SASA UMEPILIZA
MWANAMITINDO na mtangazaji mahiri Bongo, Jokate Mwegelo amezua utata baada ya kupiga picha akiwa ametinga suruali iliyochanika.
Akizungumzia picha hiyo ambayo imevuja
katika baadhi ya mitandao, Jokate alisema alivalia mavazi hayo hivi
karibuni Afrika Kusini alipokuwa amekwenda kurekodi wimbo wake mpya
(hakuutaja jina) na alivaa makusudi ili kuonesha utofauti.
“Nimeamua tu kuwa tofauti maana hata
watu wengi walikuwa wakijiuliza kulikoni mimi kuvaa hivyo lakini mimi
nafikiri lazima kuna wakati tunatakiwa kuonekana tofauti na siyo mapambo
muda wote ukibadilika hata unachofanya unakuwa tofauti,” alisema
Jokate.
0 comments: