Tcu yakifungia chuo cha IMTU kudahiri wanafunzi wapya
Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania imesitisha udahili wa wanafunzi wapya katika chuo kikuu cha IMTU kwa mwaka wa masomo 2014/15 na kukipa muda wa miezi 3 chuo hiko kurekebisha kasoro zinazojitokeza mara kwa mara ikiwemo kudahili wanafunzi wengi.
Akizungumza
na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Kaimu katibu mtendaji
wa Tume ya Vyuo Vikuu Prof. Magishi Mgasa amezitaja kasoro nyingine
zilizopelekea tume hiyo kukifungia udahili chuo hicho ni pamoja na
kuendesha program ya ngazi ya cheti bila ya ithbati ya TCU sambamba na
kukaidi agizo lilitolewa na Tume hiyo la kusitisha programu hiyo.
0 comments: