CHID BENZ AACHIWA KWA DHAMANA
HATIMAYE
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Rashid Makwiro 'Chid Benz' leo
asubuhi amepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya kesi yake ya
kukamatwa na dawa za kulevya.
Msanii
huyo, jana alipandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu ya kukutwa na
madawa ya kulevya ambapo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana ya
shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili wasiokuwana hatia.
Kesi yake itasikilizwa tena Novemba 11 mwaka huu.
0 comments: