CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHAKANUSHA TAARIFA YA DIAMOND KUTUNIKIWA PHD
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Rwekaza Mukandala
amekanusha taarifa zilizozagaa zinazodai kuwa msanii wa Bongo Fleva
Diamond Platnumz atatunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) kutokana na
mchango wake kwa jamii.
Akizungumza
na Power Jams ya East Africa Radio, Prof. Rwekaza Mukandala ambae yupo
nje ya nchi kwa sasa amesema taarifa hizo si za kweli ni uzushi tu.
“Hizi
tetesi ni za uvumi, si za kweli,” alinukuliwa na mtangazaji wa radio
hiyo ambapo alidai walishindwa kuelewana vizuri kutokana na mawasiliano
kuwa si mazuri.
Hivi
karibuni kwenye mitandao ya kijamii iliibuka taarifa iliyosema: Katika
mahafali ya 44 ya Chuo Kikuu Dar es Salaam yatakayofanyika katika Ukumbi
wa Mlimani City tarehe 08 November 2014, aliyekuwa mkuu wa chuo
(Chancellor) wa UDSM marehemu Balozi Fulgence Kazaura na msanii maarufu
Afrika aliyeshinda tunzo nyingi zaidi kuliko wasanii wote Tanzania
Diamond Platinumz watatunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Heshima (Honoris
Causa) ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa mchango wao kwenye jamii.
0 comments: