HII HAPA TAARIFA KAMILI YA KUHUSU WAZUNGU RAIA WA AFRIKA KUSINI WALIOKUTWA WAMEKUFA CHUMBANI JIJINI DAR
WAZUNGU wawili ambao ni mume na mke wanaodaiwa kuwa ni raia wa Afrika Kusini, wamekutwa wamekufa chumbani kwao katika nyumba waliyokuwa
wakiishi maeneo ya Slipway, Masaki jijini Dar es Salaam Jumatano
hii.Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa wawili hao ambao walikuwa
wakifanya kazi katika baa iitwayo Mashua iliyo ndani ya Slipway, huku
mwanamke, aliyetajwa kwa jina la Hotsan, akiwa ndiye Meneja, walikutwa
chumbani kwao wakiwa wamefariki baada ya kutoonekana kazini tokea
Jumanne, siku ambayo Watanzania walikuwa wakikumbuka miaka 15 baada ya
kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Inadaiwa
kuwa baada ya kutotokea kazini katika muda wa kawaida, wafanyakazi
wenzao walijaribu kupiga simu zao za mikononi, lakini zote zilikuwa
zikiita pasipo kupokelewa karibu mchana kutwa na hivyo kuwapa maswali
mengi yasiyo na majibu.
Siku iliyofuata, inadaiwa kuwa wafanyakazi wenzao walipojaribu tena kupiga namba hizo, simu zote mbili hazikupatikana.
Jeneza lingine likitolewa ndani ya chumba hicho.
Awali,
walihisi huenda wenzao wameamua kuacha kazi baada ya kupata sehemu
nyingine, lakini baadaye wakafikia uamuzi wa kuwafuatilia nyumbani kwao
ili kujua kilichotokea.
Walipofika,
walikuta milango ikiwa imefungwa kwa ndani, kitu kilichowafanya waamini
kuwa walikuwa ndani. Kwa kushirikiana na majirani, wafanyakazi hao
waliamua kuvunja mlango wa chumba wanacholala wanandoa hao na kuwakuta
wakiwa kitandani wamelala, kila mmoja akiwa amegeukia upande wake.
Baada
ya kuona tukio hilo la kushtusha, waliamua kuwaita Polisi ambao
walipofika na kuiona miili hiyo, waliamua kuwaita wenzao wa kitengo
maalum cha uchunguzi (Crime Investigation) ambao baada ya kufika,
waliwataka raia na majirani waliokusanyika hapo kukaa mbali ili
kuwapisha kufanya uchunguzi.
Kamanda Suleiman Kova.
Askari
hao walikaa na miili ya marehemu kwa zaidi ya saa tatu wakiwafanyia
uchunguzi na baada ya kukamilika kwa zoezi hili, miili hiyo ilichukuliwa
kupelekwa hospitalini Muhimbili.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuwataja marehemu kuwa ni Roxxana Hilari na Hainess
Hilton William na kwamba uchunguzi zaidi juu ya kilichowaua unaendelea.
0 comments: