LICHA YA KUPIGWA STOP, DAVIDO NDANI YA JUKWAA MOJA NA T.I LEADERS CLUB KWENYE SERENGETI FIESTA 2014




Msanii TI akiingia katika Ukumbi wa Bongoyo uliopo katika Hoteli ya Sea Cliff Jijini Dar Es Salaam kwaajili ya kufanya mkutano na waandishi wa Habari kabla ya kupanda kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta muda mfupi ujao

Baadhi ya wasanii kutoka mataifa mbalimbali ambao watapanda katika jukwaa la Serengeti Fiesta leo

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Bw Steve Ganon akiongea na wanahabari leo katika ukumbi wa mikutano wa Bongoyo uliopo katika Hoteli ya Sea Cliff Jijini Dar wakati timu nzima ya Serengeti na Prime Time Promotions ambao ndio waandaaji wa Tamasha la Fiesta walipokuwa wakimtambulisha msanii nguli kutoka Nchini Marekani TI kabla ya kupanda jukwaani Muda mfupi ujao katika Viwanja vya Leaders.


Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Ephraim Mafuru akitoa machache wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bw Joseph Kusaga akitoa machache kabla ya kumtambulisha Msanii wa Muziki Kutoka Nchini Marekani TI ambae atapanda kwenye jukwaa la Fiesta muda mfupi ujao katika Viwanja vya Leaders.

Msanii kutoka nchini Nigeria Davido akiongelea jinsi atakavyo wapagawisha watanzania leo katika jukwaa la Serengeti Fiesta muda mchache ujao katika viwanja vya Leaders.
Wanahabari wakiwajibika wakati wa mkutano wa Kumtambulisha Msanii TI ambae atapanda katika jukwaa la Serengeti Fiesta leo katika Viwanja vya Leaders.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

0 comments: