Msiba mwingine tena leo baada ya YP tumeondokewa na mwigizaji. Sherry
Ni
masaa machache tu yamepita tangu muziki wa kizazi kipya Tanzania, Bongo
Fleva kumpoteza aliyekuwa staa wa muziki huo kutoka kundi la TMK
Wanaume Family, aliyekuwa akifahamika kwa
jina la YP, taarifa nyingine
ya simanzi inahusu msiba wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo Muvi.
Katika ukurasa wake wa instagram, muigizaji na mchekeshaji maarufu
anayefahamika kwa jina la Kitale ama Mkude Simba (@mkudesimbaoriginal),
amepost picha ya muigizaji Shery Mwana aliyefariki masaa machache yaliyopita.
Msanii
'YP' toka kundi la TMK Wanaume Family amefariki dunia jana usiku katika
hospitali ya Temeke ambako alikuwa akipatiwa matibabu akisumbiliwa na kifua kwa muda mrefu
lakini hali ilikuwa mbaya katika wiki mbili kabla ya kifo chake.
Meneja wa TMK Wanaume Family Said Fela amethibitisha kutokea kwa msiba huo. Msiba wa msanii huyo uko Keko nyumbani kwa baba yake.
Said Fella amesema Marehemu ambaye jina lake halisi ni Yessaya Ambikile alifanya vizuri na msanii mwingine Y Dash na nyimbo kama 'Ulipenda Pesa', 'Pumzika', 'Shemsha' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume Family kama 'Twende zetu' ya Chege, 'Dar mpaka Moro', 'Kichwa kinauma', 'Tufurahi' na nyimbo nyingi za TMK Wanaume family

credit:djfetty
0 comments: