ROSE MUHANDO ADAIWA KUBWIA UNGA!


HUKU mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii, nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando bado anaandamwa na madai mazito kwamba anatumia madawa ya kulevya ‘unga’ yanayomfanya kuwa hoi kiasi cha kushindwa kutokea kwenye matamasha mbalimbali anayolipwa fedha, Risasi Jumatano linateremka nayo.
Nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando.
Kwa mujibu wa vyanzo, Rose anadaiwa kutumia unga kiasi kwamba, baada ya matumizi hujikuta akishindwa kufanya jambo lolote lile la kujitafutia mkate wake wa kila siku na ndiyo maana amekuwa akikwaa skendo za kupokea fedha za shoo halafu hatokei tu!
WATOA MADAI
Hivi karibuni, akina mama watatu walifika kwenye Ofisi za Global Publisheers na kumtolea madai Rose kuhusu tuhuma zanazomwandama kwamba amekuwa akiingia mitini na fedha za watu wanaomwita kwenye matamasha ya nyimbo za Injili.
“Sisi tunavyojua, Rose anatumia madawa, wengine wanasema unga wengine wanasema sijui nini huko. Sasa akishatumia hayo madawa huwa yanamfanya awe kama amelewa na kushindwa kufanya lolote.
“Huwa anafika hatua anashinda kitandani amelala tu na hawezi kutoka, ndiyo maana mtu anaweza kumpa pesa asitokee kuimba kwa sababu anashindwa kutoka ndani kwake.
“Kwa hiyo jamani, si suala la kumwandika tu kwamba anaingia mitini na fedha za watu bali mumsaidie Rose kama kweli mnampenda, sisi wenyewe tunamwombea kwa Mungu kila siku,” alisema mama mmoja kati ya hao waliofika lakini bila kutaja majina yao.
MADAI SUGU
Madai ya kwamba, Rose anatumia madawa ni ya siku nyingi, wengi wamekuwa wakisema wana uhakika, wengine wanasema wanasikiasikia tu lakini hawana uhakika.
Mratibu wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama.
Magazeti ya Global (Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi Jumatano, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi) yameshapokea madai hayo kwa muda mrefu lakini kilichokuwa kikifanyika ni kuendelea kumchunguza msanii huyo kuhusu madai hayo.
RISASI LAINGIA KAZINI KUCHUNGUZA
Kufuatia madai ya akina mama hao waliojitambulisha ni waumini wa kutoka katika kanisa moja la kilokole jijini Dar, gazeti hili liliamua kuingia kazini kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli au uongo wa madai hayo.
WATU WA KARIBU NA ROSE
Mtu wa kwanza kumtafuta ambaye gazeti hili liliamini kwamba anaweza kujua chochote kuhusu madai hayo ni mratibu wa Tamasha la Pasaka linalofanyika kila mwaka kwenye baadhi ya mikoa, Alex Msama.
Msama: “Mimi siwezi kusema ni kweli kwani sijawahi kumwona akitumia wala sijui kama ameathirika.”
Risasi Jumatano likamsaka Katibu wa Chama cha Waimba Injili Tanzania (Chawaita), Stela Joel: “Mimi sijui, kama unasema kuna watu wamekuja ofisini kwenu na kutoa madai hayo, basi wamwombee. Lakini tutachunguza.”
MCHUNGAJI
Risasi Jumatano pia lilibahatika kuzungumza na mchungaji mmoja (jina tunalo) ambaye alisema ameshawahi kusikia taarifa hizo akamuuliza Rose lakini alimkatalia kuwa si madai ya kweli.
“Ila ninachojua mimi ni kwamba, Rose amekuwa akitumia dawa f’lani (akazitaja jina). Hizi ni dawa zinazopatikana kwa njia ya sindano. Mara nyingi mtu akiwa hajiwezi kwa maana ya kushindwa kufanya kazi anachomwa hizi zinampa nguvu.
“Niliwahi kusikia kwamba, kuna daktari mmoja katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (akamtaja jina). Huyu ndiye aliyekuwa akimchoma sindano zenye dawa hizo Rose pale mwili unapokuwa dhaifu.
Baadhi ya madawa yaliyowahi kukamatwa.
“Ila madhara yake sasa, dawa ikiwa imekwisha mwilini, mtu anakuwa mlegevu, anahisi kizunguzungu au kulalalala, kutokwa jasho jingi na kuhisi anaumwa kiasi kwamba ukimwona unaweza kusema ni teja. Ni dawa ghali sana kwa dozi moja, nadhani ni shilingi laki sita,” alisema mchungaji huyo.
Akaongeza: “Nasikia Rose amefika mahali huwa anajichoma mwenyewe akipata dozi. Kwa hiyo kwa suala la kubwia unga nadhani alilikanusha.”

ROSE MWENYEWE SASA
Risasi Jumatano, juzi lilimpigia simu Rose lakini hakupokea hata baada ya kurudia kumpigia mara kadhaa. Likamtumia meseji na kumsomea mashitaka yote, akajibu:
“Samahani sana nawaomba mnipumzishe kuniandika...najua ni nani na kwa nini ananitenda hivyo, ni kwa sababu anataka kunitumia kwa faida yake na ni mtu hatari sana kwangu na kwa taifa zima.
“Mtu huyo anafanya haya ili kuniziba mdomo kwani najua siri zake nyingi na nzito, nashindwa kusema ataniua.”
Hata hivyo, Rose alipotakiwa kumtaja kwa jina mtu huyo ambaye Risasi Jumatano halimjui, alikataa katakata akisema anaogopa!

0 comments: