SI KILA MWANAMKE ANASTAHILI KUWA MKE,HEBU ONA HII UTAKUBALI.

 



Kuna msemo usemao bora ukosee kujenga nyumba kuliko kukosea kuoa,msemo huu unamaana sana kwani husisitiza umuhimu wa kufanya uchaguzi sahihi wa mtu ambaye unatarajia awe mkeo maana huyu ni mtu wa pekee ambaye utakuwanae maishani mwako kwenye shida na raha sasa kama ukibugi utajuta kuzaliwa.
Hebu tuone sifa kadha za mtu mwanamke ambaye anastahili kuwa mke kwani si kila mwanamke anasifa za mke.
*Awe na tabia nzuri,yaani vitu kama hila,uvivu,kinyongo au udokozi kwake vikae mbali kwani vinginevyo atakuwa mzigo na muda wowote ukiwanae kama mkeo atakuaibisha.
*Awe mvumilivu na asiwe mwepesi kukukatisha tamaa kwani katika maisha kuna mambo magumu ambayo kiukweli bila kukaza moyo.
*Awe mwenye maadili mema na yanayokubalika katika jamii,sio mavazi ya ajabu ajabu mithili ya kidada kinachouza mwili wake.
*Awe mwenye sura nzuri ambayo inakuhamasisha kuwa nae wakati wote kwani mvuto ni miongoni mwa jambo la msingi ili kuhakikisha unabaki njia kuu.

0 comments: