Wema Sepetu Sasa Ajuta Kuwa Maarufu, Asema Umaarufu Unamtesa
‘BEAUTIFUL Onyinye’, WEMA Isaack Sepetu
‘Madame’ ametoa ya moyoni na kufichua kwamba maisha yake ya umaarufu
anayoishi yanamtesa kwa asilimia 40.
Pamoja na mateso hayo, staa huyo wa
filamu alisema anafurahia maisha yake kama mtu maarufu ikiwamo na
kuandikwa na vyombo vya habari mara kwa mara.
“Kuna wakati najutia kuwa maarufu kwa asilimia kama 40 hivi lakini nashukuru kwani kwa asilimia 60 nayafurahia maisha yangu.
“Ukiwa nyota kuna changamoto nyingi
sana, kuna wakati mtu anaweza kukuandika habari inayokufanya ushindwe
hata kutoka nje na kubaki ndani tu,”alisema.
Wema alisema kuna wakati huwa anatamani
asingekuwa maarufu kwani akifanya kitu kidogo hata kama ni cha kawaida
lakini hupokelewa kama habari kubwa na kuongelewa sana.
“Lakini katika maisha kama haya sina cha kufanya japo kuna mambo ambayo huniumiza na najitahidi sana kuvumilia,” alisema.
0 comments: