AIBU TUPU: KIVAZI CHA KIHASARA CHA MSANII AMANDA WA BONGO MUVI
Mpenzi Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Moja Kwa Moja
Msanii
wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina
yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha
wazi makalio yake.
Msanii wa filamu, Tamrina Posh
‘Amanda’ akiwacharukia wanaume waliokuwa wanampigia miluzi huku
wakimzodoa. Tukio hilo lililowashangaza wengi lilijiri eneo la Mwenge
Bamaga jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa akitembea kuelekea kwenye
mgahawa uliopo eneo hilo.
Huku akitembea kwa staili ya
‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani
kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza
mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.
‘Amanda’ akiingia kwenye gari
kuondoka Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume ambao wengi wao ni
madereva wa Bajaj na mafundi gereji walionekana kumzodoa huku wakieleza
kuwa, ni msanii asiyejiheshimu.
“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo
nini? Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale
wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa
tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.
Tamrina Posh ‘Amanda’ akipozi. Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni hicho, mwandishi wetu alimfuata Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote aliingia kwenye gari na kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara waliokuwa wakimpigia miluzi. Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila kupokelewa
0 comments: