Wasikilizaji
wa kipindi cha ‘Genge’ cha 93.7 E-FM ya Dar es Salaam wamepokea kwa
masikitiko taarifa kutoka kwa mtangazaji wa kipindi hicho waliyekuwa
wamemzoea, Penniel Mungilwa a.k.a VJ Penny kuwa hatasikika tena kwenye kipindi hicho.Kupitia Instagram Penny ameandika:“Gengerzzz hata sijui nianzie wapi, ila wacha niwaambie nawaona nyie wote kama familia
yangu…toka day 1 mmekua na bonge la support! Message zenu ndio zilikua
zinatuunganisha kama tunajuana…sina cha kuwalipa! I love u all beyond
words!.. Sasa time yangu ya kufanya Genge imekwisha, ila sio ndio
muondoke kimoja.. Mpeni support jamaa anaefuata, project zingine kali
zinakuja ntawasanua, si mnajuanga napenda kuwapa vitu flani flani
AMAZING??? I SALUTE ALL OF U…camp,unit, crew zote! Wadau wote
mlitisha…kila jambo lina mwanzo na mwisho! Nimemaliza kazi yangu ya
Genge..na wote mjipongeze kwa pamoja tulifanya vitu AMAZING…ALUTA
CONTINUA! Baraka tele kwenu GENGERZ”
0 comments: