INASHANGAZA NA KUSIKITISHA SANA HUYU NDIO MTOTO ALIYEZALIWA ANASEHEMU ZA SIRI 4
A SIRI 4
Mpenzi Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Moja Kwa Moja .
Gazeti hili linawashauri wazazi wa mtoto huyo kurudi KCMC kumchukua
mtoto huyo. Kiumbe huyo ni malaika na hana kosa lolote. Uwazi
linaendelea kumfuatilia mtoto huyo hatua kwa hatua na litakuwa linatoa
ripoti ya maendeleo yake.
AGANO
kwamba nyakati za mwisho, matukio mengi ya ajabu yatadhihirika,
linazidi kupata nguvu kutokana na tukio la kusikitisha lililotokea
Arusha.
Wakazi wa jiji hilo, wanaliita A-Town na ukifanikiwa kushiriki vijiwe
mbalimbali, utabaini jinsi mkoa huo ulivyozizima kutokana na kuzaliwa
motto mwenye sehemu nne za siri.
Kila kona ya jiji hilo, anazungumzwa mtoto huyo kwa hali ya mshangao.
Malaika huyo wa Mungu hajapewa jina lakini mama yake anaitwa Naishooki
Logolie, 23, mkazi wa Kijiji cha Injok, Wilaya ya Arumeru, Arusha.
Kutokana na habari ya mtoto huyo kupata umaarufu mkubwa, huku wengi
wakitaka kumjua zaidi, Uwazi lilimsaka mtoto huyo na kubaini maajabu
mengine kwamba mbali na sehemu hizo za siri pia ana miguu mgongoni.
Kwa ushuhuda wa Uwazi, mtoto huyo ni wa kiume lakini ana sehemu za
siri nne, tumboni, mgongoni, ubavuni na kwenye eneo la kawaida.
KAULI YA MAMA MZAZI
Uwazi lilifanikiwa kuzungumza na Naishooki ambaye alisema: “Mwanangu
nilimzaa kwa njia ya upasuaji kwenye Hospitali ya Olturumet, Halmashauri
ya Arusha.”
Naishooki alisema hajui ni mtihani gani umempata kwani hakuwahi
kuhisi tatizo lolote tumboni. Baada ya hapo, mwanamke huyo aliangua
kilio na hakuweza kuzungumza tena.
Mama mzazi wa Naishooki (bibi wa mtoto huyo), Naishiye Logolie, alisema kuwa ni tukio la ajabu mno kutokea.
“Mtoto wangu akiwa mjamzito, hakuwahi kuonesha dalili za tatizo. Tumeshangaa kuona maajabu haya,” alisema Naishiye.
KAULI YA DAKTARI
Akizungumza na waandishi wa habari, Mganga wa Halmashauri ya Arusha,
Dk.Thobias Mkina alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa
wanajaribu kufanya linalowezekana kuokoa maisha ya mtoto huyo.
“Matukio ya kuzaliwa watoto wakiwa na matatizo yanatokea lakini hili
kidogo linaonekana kuwa la kipekee sana kutokana na maumbile ya mtoto,”
alisema Dr.Mkina.
Alisema kuwa sababu za kitaalamu zinazoweza kusababaisha matukio ya
aina hiyo ni matumizi ya dawa zenye kemikali wakati mama akiwa
mjamzito.
Dokta huyo aliongeza, wakati mwingine kuna matukio ya kurithi kutoka kwa kizazi cha mhusika.
Hata hivyo alisema uchunguzi unaendelea na wakimaliza kwa upande wao watampatia rufaa kwenda katika hospitali kubwa zaidi.
MTOTO ATELEKEZWA
Taarifa za baadaye zinasema kuwa mtoto huyo aliepelekwa Hospitali ya
KCMC, Moshi, Kilimanjaro kwa lengo la kufanyiwa upasuaji lakini wazazi
hao baada ya kuambiwa gharama, walimtelekeza wodini.
Uwazi limejiridhisha kuwa mtoto huyo ametekezwa wodini kwenye
hospitali hiyo, huku wazazi wake wakisema kuwa hawawezi kuishi na kiumbe
huyo kwa madai kwamba ni laana kutoka kwa Mungu.
0 comments: