Janga Jingine Lamkuta Emmanuel Mbasha, inadaiwa Kaficha Habari Kuhusu Mfanyakazi wake Aliyejinyonga ndani kwake.
Majanga yanazidi kumuandama aliyekua mme
wa muimbaji maarufu Frola Mbasha, akiwa bado ana kesi mahakamani
akidaiwa kumbaka ndugu yake hili ndio janga jingine lilimkuta Emmanuel
Mbasha. Janga hilo ni la kufariki kwa mfanyakazi wake wa ndani ambae
alijinyonga ijumaa iliyopita.
Inadaiwa kua Emmanuel na mfanyakazi huyo
walikua wakiishi wawili tu ndani ya nyumba ya Emmanuel, lakini kitu cha
kushangaza zaidi ni pale mfanyakazi huyo alipojinyonga. Inavyosemekana
Emmanuel hakutoa taarifa kwa majirani kuhusu tukio hilo badala yake
alitoa taarifa polisi na kisha kuusafirisha mwili wa marehemu kwa siri
sana kwenda kumzika Singida.
Tumepata ujumbe kutoka kwa mmoja wa
majirani wa Emmanuel Mbasha ambae hakutaka jina lake litajwe, ujumbe huo
ulisema ” Kuna kijana wa kazi toka Singida alikuwa anaishi na Emmanuel
Mbasha, amejinyonga na kuacha ujumbe kuwa kwa yaliyomkuta ameamua bora
ajinyonge. Walikuwa wanaishi na Mbasha tu huko ndani na baada ya
kujinyonga Mbasha amefanya siri kubwa mno hawakuweka hata msiba. Kijana
alijinyonga Ijumaa na ndugu wakatafutwa wakaenda kureport polisi kwa
ajili ya mazishi na wamemsafirisha kwenda kuzika Singinda. Mbasha hakuta
majirani tujue. Mnaweza mtafuta kwa maelezo zaidi maana nikiandika hapa
yeye ndo mwenye ukweli alimfanyia nini kijana wa watu.”
Bado tunafanya jitihada za kumtafuta Mbasha kwa ajili ya kuzungumzia suala hili…
0 comments: