KAMANDA KOVA AHUSISHWA NA FREEMASON
KIMENUKA! Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, CP Suleiman Kova, wiki iliyopita alifunguka kuwa, kuna watu
wamekuwa wakimhusisha na imani ya Freemason.
Kamanda Kova aliyasema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama
wa mkoa wake kuelekea Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
“Wananchi wanatakiwa kuwa makini na hawa watu ni hatari sana,wamekuwa
wakitoa namba zao za simu na kuwatangazia wananchi wanaotaka kujiunga
nao ili wawe matajiri wapige namba walizotoa ili wajiunge baada ya kutoa
fedha, nashangaa hata mimi watu wameshawahi kuniita Freemason wakati
siyo kweli,” alisema Kamanda Kova.
“Kwanza ninavyojua mimi Freemason anakuwa tajiri, anakuwa na mali
nyingi sasa mimi nina mali gani mpaka watu waseme ni Freemason?”
aling’aka Kamanda Kova. Kova hakufafanua ni kwa nini amekuwa akiitwa
Freemason ingawa aliwataka wananchi wajihadhari na imani hiyo.
“Polisi wanatoa tahadhari kwa wananchi kwa watu wanaojiita Freemason
na kutoa namba zao, hawa ni hatari sana, ni matapeli, hawafai ndani ya
jamii, watashughulikiwa,” alisema Kova.Katika mkutano huo na waandishi
wa habari Kova alisema kwamba msako mkali umeanza dhidi ya wahalifu na
wale wote wanaovunja sheria ikiwa ni pamoja na madereva wa pikipiki na
magari.
0 comments: