SATAKA LA MISS TANZANIA 2014,UNAAMBIWA SITTI MTEMVU AINGIA MITINI,ASWAKA USIKU NA MCHANA BILA MAFANIKIO
WAKATI suala
la kudaiwa kudanganya umri likiwa bado ‘bichii’, taarifa zinadai kuwa
mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu ametoweka na hajulikani
alipo, Risasi Mchanganyiko limechimbua stori kamili.
Mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Shughuli ya kumsaka mrembo huyo ili kujua undani wa sakata lake ilianzia Temeke ambako ilielezwa kuwa ndiko anakoishi.
Mapaparazi wetu walipofika katika nyumba
waliyoelekezwa, walikuta imebadilishwa na kuwa Ofisi ya Vikoba ambapo
mmoja wa wahudumu wa ofisi hiyo kwa sharti la kutoanika jina lake
gazetini, aliwataka waandishi wetu kwenda Mbezi-Makonde akidai ndiko
anakoishi kwa sasa.
“Hapa ilikuwa nyumba ya zamani lakini
kwa sasa ni ofisi na Sitti hakai hapa, kama mnamtaka nendeni
Mbezi-Makonde huko nasikia ndiko anakoishi,” alisema mtumishi huyo.
Mapaparazi wetu hawakuchoka, walifunga
safari hadi Mbezi-Makonde ambapo walikuta nyumba yenye maduka
yaliyoandikwa Mtemvu Foundation, wakaenda moja kwa moja katika saluni
mojawapo iliyokuwa na bango lililosomeka Malisa huku likiwa na picha ya
Sitti sambamba na namba za simu.
Sitti Mtemvu wakati wa kutwaa taji la Miss Tanzania 2014.
Dada mmoja aliyeonekana kufanana na
Sitti alizidi kutibua hali ya hewa baada ya kusema Sitti amesafiri nje
ya nchi pasipo kufafanua nchi gani.“Sitti amesafiri nje ya nchi, ila
kama mnamtaka nafikiri nitawapa namba zake akirudi kati ya Jumatatu au
Jumatano ya wiki ijayo (wiki hii),” alisema dada huyo pasipo kutaja jina
lake.
Mmoja wa majirani wa mrembo huyo alihoji
inawezekanaje mrembo huyo akasafiri nje ya nchi wakati suala lake la
umri halijapata ufumbuzi?“Mh! Ataondokaje wakati bado ana majanga ya
umri?” alihoji jirani huyo.
Aidha, mapaparazi wetu hawakutaka
kuishia hapo, Jumapili iliyopita walitia timu Buza Kipera katika Kanisa
la The Revelation Church la Nabii Yaspi Bendera ambalo ilielezwa kuwa
Sitti anaabudu, ili kujiridhisha kama yupo, lakini pia hakuonekana huku
waumini wakidai hawajamuona kwa siku za karibuni.
Nabii Yaspi Bendera wa Kanisa la The Revelation Church.
“Hatumuoni siku hizi, ila alikuwa
anakuja katika ibada ya peke yake kwa nabii saa kumi lakini siku za
karibuni hatumuoni,” alisema muumini mmoja.Katika ibada inayoendeshwa
kanisani hapo ambayo mapaparazi wetu walizama ‘kiintelijensia’, Nabii
Yaspi alisikika akimkingia kifua Sitti kuwa alistahili ushindi na
kumtabiria kufika mbali na hata kuwa Miss World huku akiwaonya
wanaomfuatilia mrembo huyo.
“Mara ya kwanza nilimtabiria Sitti
kushinda u-miss Tanzania na kweli akashinda, sasa wanatokea watu wakidai
mara ana hipsi kubwa, ooh kadanganya umri, huu wote ni upepo tu na
utapita.“Kama Sitti hatakengeuka kwenye imani yake atafika mbali zaidi
na kushinda hata Miss World. Wale wote watakaoendelea kumfuatilia
wataparalaizi,” alisema Nabii Yaspi.
Hadi mwishoni mwa wiki iliyopita, Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), walisema bado wanalifanyia
uchunguzi suala la Ritta kudaiwa kufoji cheti cha kuzaliwa kutokana na
baadhi ya nyaraka zake kuonesha amezaliwa mwaka 1989 huku yeye akidai
amezaliwa 1991.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akitafakari jambo.
Wakati RITA na BASATA wakiwa hawajatoa tamko lolote kufuatia uchunguzi waliodai wataufanya, gazeti hili lilifanya
jitihada za kumtafuta Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara ili azungumzie sakata hilo.
“Waziri ni mtu mkubwa sana kuzungumzia
suala kama hilo, watafute wasaidizi wangu pale wizarani watakuambia
kinachoendelea. Naweza kutoa tamko halafu nikaonekana mtu wa ajabu,
kumbe watu wanaendelea kulifanyia kazi, nenda kamuone Mkurugenzi wa
Utamaduni atakusaidia,” alisema Waziri huyo alipozungumza nasi kwa njia
ya simu.
0 comments: