AUNTY LULU AMWAGA CHOZI BAADA YA KUTENDWA
MWIGIZAJI wa
sinema za Kibongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa
ametendwa vya kutosha na marafiki hivyo kwa sasa hahitaji tena kuwa na
rafiki.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Aunty Lulu alisema kwa nyakati tofauti
marafiki wamemponza akaachika kwenye uhusiano wa wapenzi wake,
kumgombanisha na watu anaofanya nao kazi na mambo mengi yanayofanana na
hayo hivyo kwa sasa hahitaji marafiki.
“Nimetendwa sana na marafiki, bora niachane nao niishi kivyanguvyangu,
nijitafutie maisha yangu mwenyewe. Sihitaji kabisa marafiki kwa sasa,”
alisema Aunty Lulu.
0 comments: