DARASA LA MAPENZI:JIFUNZE MBINU NNE ZA KUFANYA ILI USIACHIKE AU KUSALITIWA NA MPENZI WAKO
Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, mapenzi yanachukuwa sehemu
kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.Tunafanya kazi usiku na mchana
lakini pesa tunazopata tunazitumia kwenye kufurahia maisha na wapenzi
wetu.Ndiyo
maana ukiwa hauko sawa kimapenzi, namaanisha ukiwa huna mpenzi wakati
unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha, hata mambo mengine
huwezi kuyafanya kwa ufasaha.
Lakini yule ambaye maisha yake ya
kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka kutoka kwa mpenzi wake,
utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na furaha haikauki.Wakati
ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila siku kwa sababu ya
kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao. Kuna ambao kusalitiwa
kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa sababu hawajui yapi wayafanye ili
wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao.
Kimsingi nimegundua wengi hatuna elimu ya kutosha juu ya mapenzi.
Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu ambaye yuko mbali lakini hajui
wanawezaje kulidumisha penzi lao. Mmeoana wote mnafanya kazi na ni
wanandoa, mnawezaje kuishi katika msingi sahihi? Hayo yote utayajua
endapo tu utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu
kuhusu mambo hayo.
Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi kujihusisha kimapenzi, leo
umeingia kwenye uhusiano na hujui chochote, kama huna elimu ya mapenzi
hata kama umzuri vipi, utaachika tu kama siyo kusalitiwa kila siku.
Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili kama ulikuwa hujui, uanze leo
kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba. Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi
ya kiutu uzima, yale ambayo huwezi kufundishwa shuleni, kusoma kwenye
magazeti, kuona kwenye vipindi vya kawaida vya televisheni au
kusikisiliza redioni. Mtandaoni
Mitandao imekuwa ni msaada sana katika ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo
utalihitaji usilipate kwenye mtandao. Kwa maana hiyo basi, kama kuna
jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi, kuwa rafiki wa mitandao husika.
Kwa mfano unataka kujua jinsi unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako
mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao, utakuletea.Licha ya kwamba lugha
unayotumika ni ya Kiingereza, naamini wengi wetu tunajua hata kama ni
cha kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada ukiandika kwa Kiswahili pia
unaweza kuzipata.
Majarida maalum
Yapo majarida yanayozungumzia
mapenzi kwa undani wake ambayo yanauzwa sehemu maalum kwa jili ya watu
wazima tu. Kama kweli wewe ni mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo,
ukiulizia utayapata kwani huwezi kuyakuta yanauzwa kiholela.
Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa lakini elimu utakayoipata ni kubwa
na huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la
shilingi 50,000 na ndani yake ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na
mpenzi wako, namna na kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi
wako muwapo faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo
ukilinganisha na gharama ulizotumia kwenye harusi yenu?
Ongea na wataalam
Kuna wataalam wa mambo ya
mapenzi ambao wanaweza kukusaidia. Kwa mfano mimi nimekuwa nikitumia
muda wangu mwingi kushauri wasomaji wangu juu ya mambo yanayowakosesha
furaha katika maisha yao ya kimapenzi.
Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi ya akina mama ambao wamekuwa
wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana kabla ya kuingia kwenye
ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza mambo sahihi kuhusiana na
mapenzi. Nilichogundua mimi ni baadhi ya watu kuwa na aibu. Hivi
unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo unajua
kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?
Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa watu wenye uchu
na elimu hasa hii nyeti, inabidi wakati mwingine wakubali kuamka usiku
na kuangalia vipindi ambavyo vinazungumzia mapenzi kwa watu wazima.Mara
nyingi vipindi hivi huwezi kuviona mchana, wanaovirusha husubiri muda
ambao watoto wamelala. Ukiwa ni mpenzi wa kuvifuatilia vipindi hivi, ni
lazima utakuwa bora kwenye uhusiano wako.
Ni hayo tu ila kama unataka kujifunza zaidi kupitia mimi, usisite
kunitafuta. Kumbuka ujanja na ubunifu wako ndivyo vinaweza kudumisha
ndoa yako lakini ukiwa unaendesha maisha yako kibubusa, kaa mkao wa
kusalitiwa kama siyo kuachwa!
0 comments: