MWANAMKE ALIEKANA DINI KUANZA KAMPENI AMBAZO ZINATEGEMEWA KUITIKISA DUNIA..
Mwanamke
raia wa Sudan ambaye alihukumiwa kifo mapema mwaka huu kwa kuikana dini
ya kiislamu ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu awasili
nchini Marekani mwezi Julai.
Meriam Ibrahim alipokea tuzo kutoka kwa shirika moja la kikristo mjini Washington lililomtunuku kwa ujasiri wake.
Kwenye
mahojiano na BBC Meriam alisema kuwa kile anachotaka kufanya ni
kuendesha kampeni kwa niaba ya wale wote wanaokabiliwa na mauaji ya
kidini.
Alihukumiwa kifo akiwa mja mzito na mahakama nchini Sudan kwa kuasi dini yake.
Kesi hiyo ilizua shtuma kali kote ulimwenguni.Bi Meriam alizaliwa na baba mwislamu lakini akalelewa kikristo na mamaake.
lakini chini ya sheria za Sudan mahakama hiyo haikutambua dini wala ndoa yake.
Alitakiwa
kubadili dini ama auawe.Akiwa amehukumiwa kifo alijifungua mwanawe
ndani ya jela,ambaye aliishi naye katika eneo hilo kwa mda.
Hatahivyo kampeni ya kimataifa ya kuitaka serikali ya Sudan kumwachilia huru ilianzishwa na kusababisha kuachiliwa kwake.
0 comments: