NILISHUHUDIA NIKICHOMWA MOTO
MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la
Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika
kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi
alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba,
huko Segerea.
Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi
namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na
rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea
Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.
“Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba
katika mfuko nikitaka kwenda kuliuza, tulipofika Segerea Seminari,
tulisimamishwa na watu ambao walitutilia shaka wakaanza kutupekua.
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima
watuadhibu. Mara akapita dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa
sisi ni wezi na kutaka wachange hela wakanunue petroli ili watuchome
moto, uzuri ni kwamba kwa kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo
mafuta,
0 comments: