UKATILI! Mwanamke Apigwa Mawe Hadi Kufa Baada ya Kufanya Mapenzi Nje ya Ndoa Huko Somalia
Mwanamke mmoja ameuawa kwa kupigwa mawe nchini Somalia na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab.
Ripoti zinasema kuwa takriban watu 200
akiwemo gavana wa eneo hilo walishuhudia watu wakimpiga mawe mwanamke
huyo kwenye mji wa Barowe.
Mwanamke huyo wa umri wa miaka 30 alikuwa ameshutumiwa kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa.
Wadadisi wanasema kuwa mauaji hayo ini
ishara ya ushawishi wa kundi la Al shabaab hata baada ya kushambuliwa na
serikali ya Somalia pamoja na vikosi vya muungano wa Afrika.
Mji wa Barowe ambao uko umbali wa kiomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu umekuwa ngome ya Al Shabaab.
0 comments: