AIBU:MCHUNGAJI ASHANGAZA WAUMINI BAADA YA KUMUACHA MKE WAKE NA KUOA KABINTI


MCHUNGAJI Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC lililoko Mbezi ya Shamba jijini Dar, amedaiwa kuoa mke wa pili aitwaye Pamela Didas Asenga akiwa na umri wa miaka 20 tu ‘dogodogo’, Risasi Jumamosi limetonywa.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari wa Kanisa la RGC akimuoa 'dogodogo', Pamela Didas.
Kwa mujibu wa chanzo, ndoa hiyo ilifungishwa na Askofu Innocent Lugagi wa Kanisa la White House la Durban, Afrika Kusini, Agosti 29, mwaka huu.
Mke mwingine wa mtumishi huyo wa Mungu anaitwa Zuwena (Catherine) aliyemuoa mwaka 1985. Lakini kuna madai kwamba, mke huyo amemwacha.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akipiga picha na mke mpya wakati wa harusi.
Chanzo chetu ndani ya kanisa hilo kilidai kwamba, mchungaji huyo aliwaambia waumini wake aliamua kumuoa Pamela kwa vile ndoa yake ya mwanzo aliifunga akiwa  Muislam na alifungishwa na shehe (hakumtaja jina).
“Alituambia Mungu amemfunulia na amempa mke mwingine mwema ambaye ni binti mbichi, watu wewee,” kilisema chanzo.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiwa mke mpya.
Habari zaidi zinasema kuwa, mchungaji huyo baada ya kutua nchini, Jumapili moja akiwa kanisani kwake aliwatangazia waumini wake, hasa wanaume kwamba kama wana wake ambao walichukuana wakati wa ‘ujinga’ na wamekaa nao kwa miaka mitatu au zaidi na hawana tabia ya Kimungu, mkorofi na mchokozi na hawajafunga nao ndoa, wawaache ili Mungu awape wake wema.
Sasa baada ya picha za mtumishi huyo kusambaa hadi kwenye mitandao, Risasi Jumamosi, juzi lilifika kanisani kwake Mbezi ili kuzungumza naye lakini hakuwepo.
Mchungaji Peter Rashid Abubakari akiongoza maombi kanisani.
Baadhi ya waumini walioweza kuzungumza na Risasi Jumamosi walionesha kushtushwa na kitendo cha mchungaji wao kumuoa Pamela lakini hawakuwa tayari kusema neno!
Baadaye mwandishi wetu alimtafuta mchungaji huyo kwa njia ya simu ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Nipo Kiluvya kikazi lakini hilo lipo ila ni jambo langu binafsi siyo la kulitangaza.”
Baadaye alimtumia ujumbe  mwandishi akiwa ameuandika hivi:
“Sanchawa mimi ni Nabii wa Mungu Yehova, uliponipigia tu kila kitu Mungu akaniambia nia yako na kusudi lako.” 
Mchungaji Peter Rashid Abubakari.
Pia Risasi Jumamosi lilizungumza na baadhi ya wachungaji wa makanisa ya kiroho Tanzania ili kuwasikia wanasemaje kuhusu kitendo cha mtumishi huyo kufunga ndoa nyingine.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao magazetini, baadhi ya wachungaji hao walimpongeza Mchungaji Peter kwamba, aliona alikokuwa na anakokwenda ndiyo maana aliamua kuchukua uamuzi huo.

0 comments: