Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba Watishiwa Maisha


Siku tatu kabla ya Bunge la Katiba kuanza kupigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, watu wasiojulikana wameanza kusambaza vitisho vya kuwatia hofu wajumbe wa Bunge hilo.

Watu hao wamesambaza vipeperushi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma usiku wa kuamkia jana, wakiwataka wajumbe kutoingia bungeni vinginevyo yatakayowapata watajuta, huku wajumbe kutoka Zanzibar wakitishiwa kwa ujumbe wa simu kupitia mtandao wa WhatsApp.

Kunani Jamani Tanzania Tunaelekea Wapi?

0 comments: