SHOCKING !MWANAMKE APIGWA RISASI NYUMBANI KWAKE AKIWA NA MUMEWE.....
MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NKUSUBILA KAMINYONGE (70) MKAZI WA MTAA WA KATI SOWETO ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI AINA YA SMG MAENEO YA MKONO WAKE WA KUSHOTO CHINI YA BEGA NA KUPELEKEA KIFO CHAKE.
TUKIO
HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 03:00 HUKO MAENEO YA
SOWETO, MTAA WA KATI, KATA YA RUANDA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA
MBEYA. INADAIWA KUWA, WATU HAO WALIVUNJA GETI LA NYUMBA NA KISHA
KUINGIA NDANI NA KUVUNJA MLANGO WA CHUMBA ALICHOKUWA AMELALA MAREHEMU NA
KISHA KUMPIGA RISASI.
WAKATI
WATU HAO WANAVAMIA NYUMBA HIYO, MAREHEMU ALIKUWA AMELALA NA MUME WAKE
AITWAYE OSIA MALAMBUGI (72) MKAZI WA MTAA WA KATI SOWETO AMBAYE
ALISHTUKA BAADA YA KUSIKIA MLIO MKUBWA WA RISASI NA KUKUTA MKE WAKE
AMEPIGWA RISASI NA WATU HAO AMBAO WALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO HILO.
HAKUNA
KITU CHOCHOTE KILICHOCHUKULIWA/KUPORWA. CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO
KUFAHAMIKA, UPELELEZI UNAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MSAKO UNAENDELEA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA
TUKIO HILI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU HAO WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
0 comments: