AIBU: MUME WA MTU ANASWA KWENYE DANGURO.....ATAKA KUUA WAANDISHI NA POLISI..MKASA WOTE HUU HAPA
NI aibu iliyoje! Mwanaume mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mume wa mtu, amekutwa ndani ya danguro moja lililopo Sinza ya Mapambano jijini Dar ikiwa ni mazingira ya kutatanisha. SOMA HAPA : |
MAJIMAMA HAWA WANA ZAIDI YA MIAKA 35 NA BADO HAWAJAOLEWA..!!WANAJIULIZA NINI?
Njemba huyo akisihi kuachiwa baada ya sakata hilo.
Ishu hiyo
ilijiri usiku wa manane wa Ijumaa kuelekea Jumamosi ya wiki iliyopita.
Awali, Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ilipokea
taarifa kutoka kwa vyanzo vyake kuwa ndani ya danguro hilo, ameingia
mwanaume huyo aliyeonekana kuwa na heshima zake na kwa vile inaeleweka
vitu vinavyoendelea, vyanzo vilikuwa na wasiwasi naye!Bila kupoteza
muda, kikosi kazi cha OFM kilifuatilia eneo hilo na kufanikiwa kuingia
ndani ya danguro hilo ambako walimkuta jamaa huyo akiwa anazungumza na
wasichana watatu ingawa haikueleweka mara moja walikuwa wakizungumzia
nini.
Mmoja wa changudoa hao akikurupushwa kutoka kwenye danguro hilo.
Baada
ya kuwaona makamanda wa OFM, waliacha mazungumzo yao na kuwatumbulia,
lakini walipoanza kupigwa picha, ukaibuka mzozo mpya baina ya watu hao
wakisaidiwa na walinzi wanaolinda danguro hilo, dhidi ya waandishi.OFM ambao walikuwa wameandamana na walinzi shirikishi ili kudhibiti usalama, walisimama kidete kutekeleza majukumu yao huku mwanaume huyo akitoa vitisho, kwamba atawaua kwa bastola waandishi, endapo hawataacha kupiga picha. Wakati akitoa vitisho hivyo alikuwa akielekea kwenye gari lake ambako alichukua kitu kinachofanana na chuma, kilichowafanya walinzi shirikishi kutimua mbio kuhofia kuuawa.
Machangudoa hao wakitiwa nguvuni.
Wakiwa
wamebaki peke yao, waandishi wetu walianza kupigwa na wasichana,
mwanaume huyo na walinzi waliokuwa na fimbo, mawe na silaha nyingine za
jadi. Baadaye mapaparazi wetu walifanikiwa kupiga simu kwa kamanda mkuu
wa OFM ambaye naye aliwasiliana na polisi waliofika eneo hilo dakika
chache mbele.Pamoja na ujio wa polisi hao, mwanaume huyo ambaye wakati huo alikuwa ameshawasababishia majeraha waandishi wetu, aliendelea kuwa mbishi, hadi baadaye alipokubali kuingia kwenye gari lake na askari kuelekea Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Njemba huyo akiwa chini ya ulinzi.
Akiwa
njiani, mwanaume huyo aliliendesha gari kwa kasi na kutaka kuligongesha
kwenye mti hali iliyomfanya askari aliyekaa mbele upande wa abiria na
bunduki kuruka ili kunusuru maisha yake.SOMA HAPA : DUNIA IMEKWISHA HII NDIO VIDEO YA WANAFUNZI WA CHUO WALIOFUMWA LAIVU WAKIVUNJA AMRI YA SITA.
Askari mwingine aliyebaki ndani ya gari na waandishi alifanikiwa kumtuliza mtu huyo ambaye baadaye alipigwa pingu na askari kuendesha gari hadi kituoni. Ili kujua nini kiliendelea, fuatilia kesho kwenye Gazeti la Ijumaa maana jamaa huyo alilala kituoni hapo tangu Ijumaa usiku hadi Jumatatu iliyopita kutokana na hali ya mwandishi mmoja kuwa mbaya.
0 comments: