AIBU:MWANAMKE AKAMATWA KWA UTAPELI JIJINI DAR
Mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la
Mwanaheri anadaiwa kunaswa kwa msala wa utapeli na kupewa kashikashi la
aina yake baada ya ‘kutaitiwa’ na wanawake wenzake ambao ni
wajasiriamali akisemekana kukomba mali zenye gharama za Sh. milioni
mbili.Mtuhumiwa (Mwanaheri) aliyenaswa kwa msala wa utapeli akiwa chini ya ulinzi wa Polisi eneo la Mlimani City jijini Dar.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari
wetu lilijiri Mlimani City jijini Dar, mapema wiki hii, mishale ya saa
10:00 jioni ambapo Mwanaheri aliwekewa mtego na wanawake hao wanaofanyia
bishara zao Kariakoo.
Kwa mujibu wa wanawake hao, Mwanaheri alikuwa akiwasumbua kwa muda mrefu bila kurejesha pesa za mali walizompatia katika kikundi chao ambacho kinajishughulisha na kuuza bidhaa za Forever Living.
“Mwanaheri aliingizwa kwenye kikundi na mama yake mdogo (jina kapuni), tukamwamini na kumpatia mzigo wa Sh. milioni mbili.Kikosi kilichomnasa tapeli Mwanaheri kikiwa kazini.

“Cha kushangaza Mwanaheri aliondoka na
hakuonekana tena, kila tukimpigia simu hapokei na mama yake mdogo
akimpigia anamtukana ndiyo maana tukampangia mpango wa kumkamata ambao
umekamilika leo,” alisema mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa
jina moja la Zainabu.
Mama huyo alidai kuwa baada ya kuona
wamekosa njia ya kumkamata waliamua kumtafuta mtu aliyejifanya kuwa ni
mteja na kumpa namba yake ambaye aliomba wakutane Mlimani City kwani
alikuwa akihitaji mzigo mkubwa.Umati wa watu wawaliokuwa eneo la tukio wakimshuhudia tapeli huyo.
“Bila aibu sijui alikwenda kutapeli kwa
nani tena akakubaliana na mteja wakutane Mlimani City ndiyo tukajipanga
na kuja kumkamata.
“Alipopigiwa na mama aliyeahidiana naye
akaja na mzigo lakini alipotuona akaanza kukimbia tena alikuwa na
wenzake, tuliamua kumkimbiza na kumtia nguvuni,” alisema Zainabu.
Hadi gazeti hili linaondoka eneo la
tukio, wanawake hao wakishirikiana na walinzi wa Mlimani City
walimwingiza Mwanaheri kwenye gari na kumpeleka kumuhoji kisha kumpeleka
polisi ili kumfungulia kesi ya madai.
0 comments: