aJALI MBAYA YA GARI LA ABIRIA YATOKEA MOSHI KILIMANJARO NA KUSABABISHA MAUTI, JIONEE PICHA HIZI



Hii ndiyo Hiace inavyoonekana mara baada ya kupata ajali


Wananchi wakiangalia Hiace hiyo iliyopata ajali



Majeruhi wa ajali hiyo wakiwahishwa hospitalini kwa matibabu zaidi



Wananchi wakiuangalia mwili wa aliyefariki katika ajali hiyo (uliofunikwa kwa kitenge katikati ya barabara)

Wananchi wakienda kushuhudia ajali hiyo na kutoa msaada kwa majeruhi.

Ajali mbaya ya gari imetokea hii leo katika eneo la KNCU barabara ya Kibosho Kirima Moshi Kilimanjaro, baada ya gari la abiria (hiace) kupata ajali huku chanzo kikidaiwa kuwa ni mwendo kasi

Kwa mujibu wa ripota wa eddy blog aliyefika eneo hilo amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 11 jioni na abiria kadhaa wamejeruhiwa na kukumbizwa hospitali kwa matibabu zaidi huku abiria mmoja akihisiwa kufariki dunia katika ajali hiyo

Hizi ni taarifa za awali na eddy blog inaendelea kufuatilia taarifa za ajali hiyo ili uzipate kwa uhakika, endelea kuwa nasi mara mara

Picha na Thade Expensive wa eddy blog, Mosh

0 comments: