AJARI MBAYA JIJINI DAR,CONTENA LADONDOKEA HIACE
Kumetokea
ajali mbaya jioni hii maeneo ya Jeti Lumo mwisho wa lami Wilaya ya
Temeke jijini Dar ambapo gari kubwa la mizigo limeangukia Daladala
iliyokuwa kituoni. Ajali hiyo imetokea wakati gari hilo semi-trailer ikikata kona pale mwisho wa lami ambapo kontena lilianguka na kutua juu ya bodi ya daladala.
Mtoa taarifa wetu amesema hali ni mbaya na bado haijajulikana idadi ya vifo na majeruhi kwa ujumla. Pia gari imepondeka sana jambo ambalo linaashiria hatari zaidi.
Kuna gari la kunyanyua makontena
limeshafika pale lakini limeshindwa kutoa msaada wa uhakika kutokana na
kuzidiwa uzito na kontena ambapo likijaribu kunyanyua kontena kushuka
chini na kuzidi kuongeza maafa.
0 comments: