Ali Kiba akanusha tetesi za kuwalipa waliomzomea Diamond Platnumz katika tamasha la Fiesta 2014 Dar es Salaam
Mkali wa jukwaa nchini, Ali Kiba
amefunguka na kukanusha madai yaliyozuka mtaani baada ya kuzomewa kwa
msanii mwenzake Diamond wakati wa tamasha la Fiesta 2014 kuwa alihusika
kwa kuwalipa watu hao waliozomea.
Kiba amesema kuwa hata hajui uvumi huo umeanzia wapi na vipi kwani hawezi kufanya kitu kama hicho, hivyo hakuna ukweli wowote juu ya tetesi hizo ila kikubwa anawashukuru wana Dar es Salaam kwa mapokezi yao kwake kwani hakutegemea na amefurahishwa sana na imemtia moyo wa kuongeza bidii na kuandaa vitu vingine vikali zaidi.

Katika hatua nyingine Kiba amesema kuwa video ya ‘Mwana’ inatarajiwa kutoka muda wowote kati ya wiki hii au ijayo kwani ipo kwa ajili ya suprise yaa mashabiki wake wa kweli na wale wote wanaosapoti muziki wake.
0 comments: