MAMA KANUMBA AMTAKA WEMA SEPETU AZAE MAPEMA KABLA AJAWA MZEE
MAMA wa
aliyekuwa nguli wa sinema za Kibongo, Steven Kanumba, Flora Mtegoa
amempa darasa la kuzaa haraka mwigizaji Wema Sepetu na mpenzi wake,
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mama Kanumba alifunguka hayo hivi karibuni alipokuwa akipiga stori na
mwanahabari wetu ambapo alipotakiwa kutoa ushauri juu ya penzi la Wema
aliyewahi kuwa mpenzi wa mwanaye, mama huyo alisema azae haraka kwani
umri haumsubiri.
“Kanumba hakuwahi kunitambulisha mwanamke yeyote zaidi ya Wema na aliapa
kumuoa, akaniambia hawezi kuniletea mwanamke mwingine, nimshauri Wema
azae na bebi wake kwani mtoto ni faraja kwake,” alisema mama Kanumba.
0 comments: