Aliyepigwa Risasi Tumboni Akiwa kwenye Gari Jana Magomeni Afariki Dunia
Juzi ilikuwa ya kwanza kuripoti tukio la mwanamme mmoja kupigwa risasi maeneo ya Magomeni Mikumi ambaye hakuweza kutambulika mara moja, lakini sasa amejulikana na kwa taarifa zilizotolewa na ndugu, jamaa huyo amefariki dunia jana afajiri akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marehemu ametambulika kwa jina la Nyakiringa Stivin (39), mkazi wa Kibaha Picha ya Ndege na mwanamke aliyekuwa naye kwenye gari ameelezwa kuwa ni mkewe, Agness Lucas. Marehemu ni fundi wa sofa na imeelezwa na chanzo chetu kuwa alikuja jijini Dar kwa ajili ya kununua mahitaji yake ya ufundi
Alipopigwa risasi maeneo ya Magomeni alikuwa akitokea Access Bank Manzese ambako alitoa fedha kiasi cha shilingi 12M. Kwa mujibu wa mkewe, mkoba uliochukuliwa na majambazi ulikuwa na shilingi milioni 10 ambazo zilibaki baada ya kufanya manunuzi maeneo ya Manzese.
0 comments: