MAKUBWA HAYA..!!! WEMA AZUA KIZAAZAA CHINA
KUONESHA ameguswa,
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ alizua kizaazaa cha aina yake
alipomtembelea mwanamitindo Jacqueline Fitizpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ gerezani nchini China.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye gereza lililopo Mji wa Macau ambapo Wema aliambatana na meneja wake, Martin Kadinda pamoja na shemeji yake, Petit Man.
Chanzo kilicho karibu na Wema kimeeleza
kuwa, Wema alipofika na kuona mazingira ya upweke ambayo Jack anaishi,
aliwaza kwa muda na kuzungumza maneno kama mtu aliyechanganyikiwa hivyo
kuwatia hofu Martin na Petit.
“Ilikuwa mshikemshike, alimmis sana Jack
sasa alipomuona na mazingira yale ya upweke ndicho kilichomchanganya
Wema lakini baadaye kina Martin walimrudisha kimawazo na hatimaye akawa
sawa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Hata hivyo, Wema amesema mazingira ya
kule ndani siyo mabaya lakini kilichomuumiza yeye ni upweke ambao anao
na watu wanaomzunguka.”
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana
akiwa amebeba madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1
katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea jijini Bangkok nchini Thailand
kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
Agosti, mwaka huu Jack Patrick ilielezwa
kuwa alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela huku kukiwa na uwezekano
wa kupunguziwa adhabu endapo ataonesha utiifu gerezani.
0 comments: