BAADA YA PICHA ZAKE AKIDENDEKA NA MKEWE,MBOWE ATOA UFAFANUZI KUHUSU SUALA LA PICHA ZAKE AKIWA NA MKE WAKE KUSAMBAA MITANDAONI
Mbowe
Ameongea haya Kuhusu hizo kwa kusema "Kwanza mke wangu alikuwa anatimiza
umri wa miaka 50 ya kuzaliwa, vilevile firstborn wetu Dudley alikuwa
amemaliza shahada yake ya kwanza Chuo Kikuu cha Sussex, Uingereza, kwa
mambo hayo mawili, tuliona ipo haja ya kufanya sherehe, ukizingatia
watoto wetu wengine wawili Nicole na
Denis walikuwa wamerejea nchini kwa sababu nao wanasoma nje ya nchi."
Siku
hiyo ya tukio ilikuwa Jumapili, tulianza kwa kwenda kanisani Azania
Front tukatoa sadaka, baada ya hapo tulikwenda Serena Hotel kwenye
Ukumbi wa Kivukoni ambako chakula cha mchana kilikuwa kimeandaliwa,
tukajumuika na ndugu wengine pamoja na marafiki.
Haikuwa
sherehe tu kusema labda nilikurupuka kumbusu mke wangu, ilikuwa sherehe
ya kifamilia, kumpongeza mke wangu na mtoto wetu, alisema Mbowe.
0 comments: