Baada ya Uvumi wa Kuwa na Ujauzito wa Diamond,Meninah Kayazungumza Haya

Meninah ambaye ni zao kutoka Bongo Star Search miezi michache iliyopita ameripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond Platnumz huku mwenyewe akikana mara kadhaa kila anapopata nafasi ya kulizungumza hili.
Kupitia kisehemu cha You heard kwenye kipindi cha XXL Soudy Brown amekuja na stori inayohusu hali inayosemekana anayo kwa sasa Meninah kwa kile kinachosemwa ana ujauzito wa Diamond Platnumz.

Meninah ameanza kwa kusema>>’Hapana sina ujauzito,siko na Diamond pia sina mimba sina ujauzito kwani hizo habari unazitoa wapi?mimi sina mimba wala ujauzito,siko nae na sifatilii haya mambo’
Alipoulizwa na Soudy Brown kuhusu kutajwa na Diamond kama wife material Meninah amesema ‘Hapana hakuna kitu kama hicho naweza kuwa wife lakini sijawa tayari kuwa wife material.
Bonyeza play kumsikiliza Meninah akiongea na Soudy Brown.
SIKILIZA HAPA.  

0 comments: