BABA MZAZI AFUNGA NDOA NA BINTI YAKE WA KUMZAA MWENYE MIAKA 11
Wakati harakati mbali mbali za
kukabiliana na ndoa na mimba za utotoni zikiendelea na hasa katika nchi
za Afrika, baadhi ya nchi barani humo zinakabiliwa na changamoto hiyo
kupita kiasi.
Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.
Kesi ya kwanza na ya aina yake
imefanyika na hukumu yake kutolewa nchini Ivory Coast baada ya mwanamume
mmoja kumuoa binti yake wa umri wa miaka 11.
Kutokana na kitendo cha mwanamume huyo
kumuoa binti yake alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya
dola za Kimarekani mia saba.
Mwendesha mashtaka Rosine Kone amesema
kwamba kesi hiyo ya aina yake itatuma ujumbe mzito kwa raia wa nchi hiyo
ili wanaume waache tamaa.
Nao Umoja wa Mataifa unasema kwamba
ndoa za utotoni nchini Ivory Coast si suala la kushangaza, kwani mmoja
kati ya mabinti watatu huolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka kumi na
nane.
credits kwa bbc
0 comments: