BABY MADAHA ATILIA SHAKA AFYA YA ‘MKONGO WA WOLPER’
Msanii wa filamu na muziki, Baby Joseph
Madaha amesema ana wasiwasi na afya ya mwanaume Mkongo anayefahamika kwa
jina la Mwani aliyewahi kuwa mpenzi wa Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni,
Baby Madaha alisema, hofu yake hiyo inatokana na namna mwanaume huyo
anavyotapanya pesa huku akitangaza dau kubwa ili kuwapata mastaa wa
kike.
“Kimsingi mimi nina wasiwasi na afya
yake, asije akawa anataka kutumaliza. Mimi simhitaji hata kama ana
mamilioni yake. Hofu yangu ni hii tabia yake ya kutaka kutupitia sisi
mastaa, wanaokubali kuwa naye eti kisa ana mkwanja nawaonea huruma,”
alisema Baby Madaha
0 comments: