DAVINA: NATESEKA KUZUIWA KUMUONA MWANANGU
STAA wa
filamu Bongo, Halima Yahaya ‘Davina’ amefunguka kuwa yuko katika mateso
makali baada ya kuzuiwa kumuona mwanaye kwa takriban miezi mitatu na
mzazi mwenzake.
Akizungumza na mwandishi wetu, Davina alisema kabla hajaingia kwenye
ndoa yake ya sasa, alizaa mtoto mmoja na mwanaume ambaye ni dairekta
mkubwa wa filamu nchini lakini mwanaume huyo alimchukua mtoto tangu
akiwa na miaka miwili hadi sasa ana miaka mitano kila akiomba kumuona
mwanaye, hapewi ushirikiano.
“Hakuna kitu kinachouma kama mtu kunikataza kuiona damu yangu, nimebeba
mimba kwa miezi tisa halafu mwanangu hataki nimuone, nashindwa kumuelewa
sijui ni kosa gani kubwa nimefanya hadi nistahili adhabu hii,” alisema
Davina.
0 comments: