Drake ameingia kwenye headline nyingine inayohusu ugomvi, isome stori yake hapa.
Drake amekuwa moja ya mastaa ambao wamekuwa wakikaa kwenye headlines mara kwa mara kutokana na sababu mbali mbali.
Safari hii Drake ameangusha kitita kikubwa cha fedha wakati akiwa
anaharakisha kuingia ndani ya club ambapo waliomuona wanasema jamaa
alikuwa kama amekasirishwa na kitu hivi, kwa hiyo hata huko alikokuwa
anaingia huenda hakukuwa na jambo la kheri.
Staa huyo alikuwa anasherehekea birthday yake wikiendi iliyopita Club
Stadium, Washington D.C Marekani ambapo baadhi ya watu waliokuwa ndani
ya club wanasema huenda Drake alikasirishwa na kitendo cha mmoja ya
marafiki zake kupigwa na mtu asiyefahamika.
Moja ya sababu ambazo huwa zinamuweka Drake kwenye headlines ni ugomvi,
kwa hiyo kama aliingia kushiriki ugomvi wowote ndani ya club, bado si
tukio geni kwa wale wanaomfahamu staa huyo.
0 comments: