MSANII LULU AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA IITWAYO MAPENZI YA MUNGU LEO.FILAMU YAINGIA SOKONI LEO
Msanii
wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa
akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo
amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa
Kizazi Kipya Linah Sanga.
Msanii
Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha
filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari
(hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika
filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na
wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni
mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo
MAPENZI YA MUNGU.
Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya
ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa
amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.
Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa
Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo
hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea
kuwa..."Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa
Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa
yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya
Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na
watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada
ya Kuonekana katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na
FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika
Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
0 comments: