FEZA KESSY AMTAKA STTI MTEMVU MISS 2014 KUACHIA TAJI
MSHIRIKI wa
shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’, Feza Kessy, amemtaka
mshindi wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kuachia ngazi kama
kweli madai dhidi yake yanamgusa nafsi yake.
Sitti aliyeshinda taji hilo mwaka huu
katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ameibua mjadala
mkubwa katika jamii, kufuatia madai kuwa alidanganya umri wake, kwani
wakati akiwa ukumbini kujitambulisha, alidai kwamba ana umri wa miaka
18, ambao unapingwa na wadau wa kada mbalimbali
“Yeye ndiye anajua ukweli, arudishe
kiroho safi, tumche Mungu, katika maisha haya, hasa katika tasnia ya
burudani, watu wengi sana wanadanganya, huenda alifanya hivyo bila sisi
kujua nia yake, na ninaomba pia kama atafanya hivyo, watanzania
tumsamehe,” alisema Feza, ambaye pia alishinda taji la Miss Dar City
Center na Miss Ilala mwaka 2005.
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
0 comments: