Freemasons Walipasua kanisa la Anglikana
Sakata la baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicholas Mwanza (DVN) kumkataa Askofu Mkuu, Boniphace Kwangu wakimtuhumu kuwa mwanachama wa imani ya Freemason limechukua sura mpya baada ya baadhi ya waumini juzi (Jumapili) kutotokea kanisani hapo kwa madai kwamba mpaka hali ikae sawa.
Baadhi ya waumini hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe,
walisema wamepoa majumbani mpaka uongozi utoe tamko linalojulikana la
sivyo watahamia makanisa mengine kuliko kusali katika kanisa lenye
mgogoro wa kiimani.
Hivi karibuni, muumini mmoja wa kanisa hilo, Msoma Lazaro
alilazimisha kusoma tamko madhabahuni kwa niaba ya kundi lake akisema
Askofu Kwangu haruhusiwi kuendesha ibada kwenye kanisa hilo kuanzia siku
hiyo.
Hata hivyo, wakati tamko hilo likisomwa na Lazaro, kulizuka vurugu
baina ya viongozi wa kanisa hilo na msomaji wa tamko hilo wakizuia
lisisomwe kwa madai kuwa ni kuvuruga ibada kwa sababu halikufuata
utaratibu.
Akiwa katika harakati za kusoma tamko hilo, baadhi ya viongozi
walimzuia wakimtaka asubiri kwanza, lakini kutokana na msimamo wake
alilisoma tamko hilo kabla ya kuondolewa kwa nguvu na kuporwa karatasi
ya tamko hilo ambalo lilikuwa na baadhi ya picha za Askofu Kwangu.
Uwazi lilifanikiwa kupata nakala ya tamko hilo la kumkataa
Askofu Kwangu likisema kuwa ndiyo mwisho wake wa kutoa huduma zozote za
kiroho kanisani hapo na kwingineko kutokana na mambo anayotaka kuyafanya
kanisani hapo yenye ishara za kishirikina (Freemason).
Waumini waliompinga askofu huyo walisema
imethibitika kuwa ameonesha ukweli wa kuondoa zuria (kapeti) ndani ya
kanisa kwa sababu za Freemason.
Alitaka kuchimbua vigae vya madhabahuni akidai vimejengwa na kuwekwa hirizi na pia ana mpango wa kufukua kaburi la askofu hayati J. O. Rusbamayila aliyezikwa ndani ya kanisa na kulipeleka nje ya kanisa.
Alitaka kuchimbua vigae vya madhabahuni akidai vimejengwa na kuwekwa hirizi na pia ana mpango wa kufukua kaburi la askofu hayati J. O. Rusbamayila aliyezikwa ndani ya kanisa na kulipeleka nje ya kanisa.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walionekana kumtetea Askofu Kwangu
kwa kusema kuwa wanaomwandamana ni mashetani wakubwa.
Mmoja wa waumini hao, mama Mataba alisema picha zinazomwonesha askofu huyo akiwa na mwanachama wa Freemason ni za kupandikiza na za uongo, kwamba hawezi kujiunga na imani hiyo hata siku moja.
Mmoja wa waumini hao, mama Mataba alisema picha zinazomwonesha askofu huyo akiwa na mwanachama wa Freemason ni za kupandikiza na za uongo, kwamba hawezi kujiunga na imani hiyo hata siku moja.
“Picha ni za uongo.Tumekuja kusali na kuabudu hatujaja kutoa tamko
hilo hapa, hayo mambo yanatoka wapi?” alihoji mama Mataba. Aidha, mmoja
wa waumini alisema pete inayovaliwa na askofu huyo haina uhusiano wowote
na imani ya Freemason bali baadhi ya waumini wanasema bila kujua pete
ya Freemason ikoje.
Uwazi lilipozungumza na Askofu Kwangu kuhusu tamko hilo lililosomwa
kanisa hapo alisema hajui chochote kwa sababu hakuhudhuria ibada ya
siku ya tukio kwa vile alikuwa kwenye sherehe za kusimikwa kwa askofu wa
Kanisa la Africa Inland Church Tanzania ‘AICT’ ambaye hakumtaja jina.
“Hili tamko limetolewa na nani, maana sijahudhuria kanisani leo. Sisi
tulikuwa kwenye ibada ya usimikakwaji wa askofu mwenzetu. Kama
limepitia kwenye taratibu zetu halijanifikia. Kama halikupitia katika
njia hizo si sawa, ni tamko la barabarani mtu kuota na kutoa tamko,”
alisema.
Akaongeza: “Naomba nisiwe na Comment katika hilo na naomba usiniulize lolote, sielewi lolote maana sikushirikishwa na sijasali hapo.”
Cedit: Uwazi/Gpl
Akaongeza: “Naomba nisiwe na Comment katika hilo na naomba usiniulize lolote, sielewi lolote maana sikushirikishwa na sijasali hapo.”
Cedit: Uwazi/Gpl
0 comments: