SAUDA MWILIMA ANUSA KIFO
MUNGU mkubwa!
Mtangazaji wa Star Tv, Sauda Mwilima amenusurika kifo baada ya kupata
ajali ya gari maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam wikiendi
iliyopita.
Mtangazaji wa Star Tv, Sauda Mwilima.
Ajali hiyo ilitokea katika mataa ya kuongozea magari yaliyopo maeneo
hayo ambapo lori lilikosea njia na kugonga gari lake aina ya Toyota
Ipsum na kuharibika huku mwenyewe akipata majeraha mkononi na kubanwa
kifua.
“Kweli ajali ilikuwa mbaya lakini nashukuru Mungu bado ninapumua japo
nimeumia mkono na kifua, gari limeharibika vibaya lakini naamini
nitapata lingine au litatengenezwa, kikubwa bado napumua, namshukuru
sana Mungu,” alisema Sauda
0 comments: