Hii ya noti ya shilingi elfu moja Tanzania umeipata? kama bado… nimekuwekea hapa
Kumbukumbu
zako ziko sawa kuhusu yale malalamiko ya kukosewa kwa picha ya baba wa
taifa hayati Mwalimu Nyerere kwenye noti ya shilingi elfu moja? basi
kama hazipo sawa, ichukue hiyo.
Baada ya hayo malalamiko unaambiwa Benki Kuu ya Tanzania imesema imeanza
kufanyia kazi malalamiko ya kukosewa kwa picha ya Rais wa kwanza wa
Tanzania, Marehemu Mwalimu Julius Nyerere ambapo mkurugenzi wa huduma za
kibenki Emmanuel Boaz amesema tayari benki hiyo imeanza kufanyia kazi
hayo malalamiko baada ya kusoma katika mitandao ya jamii.
Mwananchi wameandika
mkurugenzi huyo alisema BoT haijapata taarifa rasmi kutoka kwa mtu
yoyote lakini wameamua kuzifanyia kazi taarifa hizo >>>“Na
sisi tumesoma katika mitandao, hakuna taarifa rasmi tuliyoipata lakini
hatuwezi kudharau tuhuma hizo na endapo tukigundua kuna matatizo
tutachukua hatua za kubadilisha haraka”
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, suala la picha kukosewa sio geni kwani
ilishawahi kutokea mara kadhaa kwa marais wastaafu na BoT ililazimika
kubadili haraka ili kutoharibu mtazamo wa Taifa ambapo alitoa mfano wa
picha ya Mwalimu Nyerere kukosewa na kuonekana nguo aliyovaa imefanana
na blauzi lakini pia picha ya Rais Ally Hassani Mwinyi ambayo ilionekana
shingoni ana mikunjo.
Kutokana na hali hiyo, mkurugenzi huyo aliwatoa hofu Watanzania kuwa
endapo itabainika kama noti hizo zina kasoro zitarekebishwa ambapo hivi
karibuni, mitandao ya kijamii iliwakariri wanafamilia ya Rais huyo wa
kwanza wakilalamikia picha hiyo kwenye noti ya Sh1,000 kukosewa.
0 comments: