IDRIS MSHIRIKI MTANZANIA BIG BROTHER ACHANGANYWA NA ‘MASSAGE’


Mwakilishi wa Tanzania kwenye Big Brother 2014, Idris Sultan.
Johannesburg, Afrika Kusini
OOIISSHH!!! Kadri siku zinavyozidi kwenda mbele katika mjengo wa Big Brother huko Afrika Kusini, ndivyo ambavyo matukio mazuri na ya kimahaba zaidi yanavyozidi kutokea. Juzikati, mshikaji wetu kutoka pande hizi alijikuta akifanyiwa ‘massage’ kabambe kutoka kwa bi shosti Goitse kutoka pande za Botswana.
Ishu ilikuwa hivi; Goitse alikuwa amemuahidi Idris kwamba angemfanyia ‘massage’ hiyo siku za usoni, kwa hiyo msela akawa na hamu ya kutaka kuchuliwa mwili wake. Time ilipofika, akajipeleka kitandani na kumwambia msela wake, Luis kwamba amkumbushe ‘manzi’ Goitse kwamba keshalala kitandani na anachokisubiria ni kuchuliwa tu.
Alichokifanya Goitse ni kumvua Idris nguo na kisha kuanza kumfanyia ‘massage’ iliyoonekana kumpagawisha sana msela kwani kwa jinsi alivyokuwa akiminywaminywa, alikuwa akitabasamu tu.
Unaweza kutazama Big Brother kwenye king’amuzi cha DSTv channel 198.

0 comments: